KWA WAFUGAJI WOTE WA KUKU WA KIENYEJI
Ndugu mfugaji wa kuku jua kwamba unaweza kuzalisha vifaranga zaidi ya mia moja kwa muda wa miezi miwili kwa kutumia wanne tu. Kuku mmoja anaweza kulalia mayai kumi na mbili au zaidi kwa wakati mmoja na atalalia mfululizo mara tatu hivyo ataangua vifaranga zaidi ya thelathini na sita kwa msimu mmoja.
Vifaranga wa kienyeji wanatotolewa kati ya siku ishirini na ishirini na moja |
wafugaji wengi wa kuku wamepoteza mamia ya vifaranga kwa kushindwa kuzingatia mambo matatu makuu
1. Usafi
2.Chakula
3.Eneo
USAFI
Vifaranga vinahitaji usafi wa hali ya juu sana kwani kinyesi chao ni sumu kwao na kina uwezo mkubwa sana wa kuwaua. safisha banda kilasiku na weka randa za kutosha kama bando ni dogo kulingana na idadi ya kuku. Unaweza kusafisha na kubadilisha randa kila baada ya siku tatu kama banda ni kubwa ukilinganisha na idadi ya vifaranga.
CHAKULA
Walishe vifaranga mara kwa mara na epuka kuwapa vifaranga pumba ya mahindi kwani yaweza kuwa sumu ya kuwateketeza vifaranga wote. Chakula kizuri kwa vifaranga ni stata na majani, mchele, dagaa nk. Safisha chombo cha chakula mara kwa mara na ni vema ukawapa chakula kidogo kidogo mara kwa mara na maji safi. Safisha chombo cha maji kila siku au mara kichafukapo na weka kiasi kidogo cha glukosi kwenye maji
ENEO
Hakikisha banda la vifaranga lipo mbali na mabanda mengine ya kuku au wanyama wengine, liwe kubwa kulingana na idadi ya vifaranga, mwanga wa kutosha na hewa safi.
By AER Poultry project
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni